Sunday, April 17, 2011

Dr SLAA ATAJA ORODHA MPYA YA MAFISADI, WAFIKIA 17

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaja orodha mpya ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Vigogo hao ni Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, John Samwel Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Philip Mangula, kwa kuhusika na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu.
Dk. Slaa alitangaza majina hayo jana mjini Tabora alipokuwa akiwahutubia wanachama na wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Chipukizi. Alisema majina hayo ni muendelezo wa yale ya vigogo wanaotuhumiwa kwa ufisadi aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambayo ni 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete.

Katika orodha ya mwaka 2007, Dk. Slaa aliwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), ambaye sasa ni marehemu, Dk. Daudi Balali, Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM) na Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM).

Wengine ni Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, kada wa CCM, Nazir Karamagi, Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM), Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM), Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na Rais Jakaya Kikwete........ BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI

CHANZO: TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment