HOFU kubwa imezuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya hatua ya uongozi wa chama hicho kuwapa muda wa siku 90 wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi. Sasa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wanataka na mwenyekiti wao aondoke nao kwenye uongozi wa chama.
Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumapili umebaini kuwa makada wa chama hicho, ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi, na ambao wamepewa siku 90 wajiondoe, wanasema ufisadi wa CCM unamgusa hata mwenyekiti wao. Wanadai naye ametuhumiwa mara kadhaa, kama wao, na kwamba amechangia kukipa chama sifa mbaya.
Wanamshangaa Rais Jakaya Kikwete, kwamba amekuwa kigeugeu, kwani alishaweka wazi kuwa kamwe hawezi kumfukuza, kumuwajibisha kiongozi wa serikali au wa chama bila ya kuthibitika kwa tuhuma zinazomkabili, ili kuepusha serikali kulipa mabilioni ya fedha iwapo mhusika atakwenda mahakamani na kushinda. Wanadai kwamba kama ni kuwajibika au chama kujivua gamba, hata Rais Kikwete alipaswa kuwa ni miongoni mwa wale wanaotakiwa kuwajibika, kwa sababu alishatajwa mara kadhaa kuhusika na ufisadi mbalimbali, ukiwemo ule wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Na wanadai kutajwa kwake huko ndiko kumeshusha heshima yake kwa umma, na hata kumfanya apite kwa shida katika uchaguzi mkuu uliopita, huku akiwa rais aliye madarakani.
Wanasema kuwa kama kutajwa mara nyingi katika kashfa za ufisadi ni kukichafua chama na ndicho kigezo kilichotumiwa na CC, NEC, Rais Kikwete hapaswi kupona kwa kuwa alishawahi kutajwa katika orodha ya mafisadi 11 na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alipokuwa akihutubia wananchi katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam........ BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment