Sunday, January 23, 2011

LIJUE KABILA LA WANYAMBO

HISTORIA YA WANYAMBO
Wanyambo ni kabila lilokuwa miongoni mwa makabila makubwa na yenye nguvu za kivita na kiuchumi. Utawala wa kibila hili ulikuwa wa kifalme ulioongozwa na wafalme “Abakama” 14 kwa nyakati tofauti. Watu wake ni wakulima na wafugaji.

Kabila la Wanyambo linapatikana katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera. Inaaminika kuwa asili ya jina la kabila hili ni eneo la Maziwa Makuu na jina la kabila hilo limetokana na aina moja wapo ya ndizi inayofahamika kwa jina la Enyambo.Aidha neno nyambo linamaanisha mtu au kitu au mmea asilia pia yupo ng’ombe wa asili wilayani Karagwe ambaye anajulikana kwa jina la Enyambo linalofahamika katika nchi za Uganda na Rwanda.

Ramani ya Mkoa wa Kagera

Himaya ya mfalme wa Karagwe ilikuwa ndiyo utawala mkubwa katika maeneo ya maziwa makuu kwa miaka kama 500 na Bweranyange Mji Mkuu wa Mfalme wa Karagwe ndipo alikaa mfalme Ruhinda wa kwanza, mwanzilishi wa himaya za Kihinda. Ruhinda alitawala eneo lote la Karagwe, Ankole, Kihanja, Ihangiro Biharamulo Bushubi na Bugufi Kaskazini, kipakana na Bunyoro na mto Mwiruzi Kusini ya Biharamulo na Mkoa wa Kigoma. Licha ya kutofahamika katika Tanzania ya leo sambamba na kupanda na kushuka kwa umaarufu wa kabila hilo. Himaya ya mfalme wa Karagwe hiyo ilitukuka na kuandikwa kwenye magazeti ya ulimwengu wakati wa wavumbuzi hususani Uingereza zaidi ya miaka 160.

                                                        Nyumba ya asili ya Kifalme

Himaya ya mfalme wa Karagwe ilikuwa ndiyo utawala mkubwa katika maeneo ya maziwa makuu kwa miaka kama 500 na Bweranyange Mji Mkuu wa Mfalme wa Karagwe ndipo alikaa mfalme Ruhinda wa kwanza, mwanzilishi wa himaya za Kihinda. Ruhinda alitawala eneo lote la Karagwe, Ankole, Kihanja, Ihangiro Biharamulo Bushubi na Bugufi Kaskazini, kipakana na Bunyoro na mto Mwiruzi Kusini ya Biharamulo na Mkoa wa Kigoma. Licha ya kutofahamika katika Tanzania ya leo sambamba na kupanda na kushuka kwa umaarufu wa kabila hilo. Himaya ya mfalme wa Karagwe hiyo ilitukuka na kuandikwa kwenye magazeti ya ulimwengu wakati wa wavumbuzi hususani Uingereza zaidi ya miaka 160.


Ufugaji ulichangia kwa kiasi kikubwa katika Uchumi wa Karagwe

Karagwe ilitumika kama njia pekee ya kufikia utawala wa Buganda kwa wageni toka Pwani na Zanzibar .Kati ya Novemba 1861 na Februari 1862 John Hannington Speke na James Grant walikaa miezi mitatu Kafuro jirani na Bweranyange na wakaandika kwa kirefu juu ya mila na desturi za Karagwe chini ya mfalme Rumanyika Orugundu Rzinga Mchuchu wa Nkwanzi ambalo ni jina la utani lenye maana ya shujaa mfuga nywele ndefu mwana wa Nkwanzi. Na kwamba kwa hivi sasa kuna hifadhi ya wanyama ya rumanyika Orugundu kuenzi mtawala huyo ambayo kwa mashariki yake katika kijiji cha Ibamba kunapatikana mto wenye maji moto ya Mutagata”anasema Tuluhungwa.


Ndizi ni Chakula kikuu cha Wanyambo

Historia ya kabila hili ilifahamika ukanda wote wa Ziwa Magharibi Victoria pamoja na nchi za Rwanda na Burundi.Kutokana na uhunzi wa mapambo mengi ya kifalme yalitengenezwa na kuhifadhiwa kwenye ngome ya mfalme.Mapambo hayo yalipendwa na mengine yalichukuliwa na Wajerumani ,walipewa zawadi na Omukama Rumanyika. Ni kabila lililoheshimika na wanyambo walijivunia Unyambo wao hali iliyoibua misemo kama, Ndyu Munyambo akala nakalenje, Omunyambo agamba echabweine.

Kabila la wanyambo ni miongoni mwa makabila makubwa Mkoani Kagera mengine ni Wanyambo wenyewe, wasubi, washubi,wahangaza,wazinga na wahaya.

SABABU NA MATOKEO YA KUPUNGUA KWA UMAARUFU WA KARAGWE

Karagwe ulianza kupoteza umaarufu wako katika miaka ya 1880 na 1890 ambapo wakoloni wa kijerumani walikuwa wakishidana kuligawana bara la Afrika huko Berlin 1884 na baadaye wakati Zanzibar na Buganda zilikuwa tawala zinazolindwa na mfamle wa Uingereza. Karagwe iliangukiwa na nuksi ambazo zilifika tawala nyingine zote kubwa katika historia kama za Alexander mkubwa utawala wa Kirumi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilikuwa vimeanza wakati Speke na Grant wakiwa Karagwe Novemba 1861 mpaka Desemba 1862 Matokeo yake ilikuwa kupungua kwa amani na kuihama Karagwe upande ulioshindwa na kupunguza wingi wa watu.


Pili ugunduzi wa njia fupi toka Mombasa kwenda Uganda kulitoa Karagwe kwenye njia Kuu ya biashara ya kimataifa na kupunguza umaarufu wake. Magonjwa ya mifugo kama ng’ombe sotoka ilishambulia mifugo ya wakazi wa karagwe katika kipindi hiki na kupunguza utajiri wa Karagwe.Wakoloni walikuwa hawavutiwi na nchi maskini.


Karagwe iliathirika kisiasa na kiutawala baada ya wafalme wake wengi kufa wakiwa wadogo bila kuacha warithi walioishafikia umri wa kutawala, ikalazimu kutawala kwa kutumia viongozi wa muda kama vile Kakoko waliotawala kwa ukatili na kuharibu himaya.

Pia Karagwe haikupewa kipaumbele katika mipango ya wakoloni wa Kijerumani kulifanya Wamisionari kutovutiwa kuweka vituo vyao Karagwe. Wamisionari wa Kikatoliki walianzisha vituo vyao Kashozi 1892, Bunena 1905, Kagondo na Rubya 1904,Katoke Biharamulo na kuanzisha shule sehemu zote hizo.Misheni ya kwanza Karagwe ilianzishwa 1934 baada ya miaka 40 baada ya kumpata Padri wa kwanza mwafrika wa kwanza Oscar aliyepadrishwa Bukoba 1917.Wa kwanza Karagwe Padri Rwakiboine alipandrishwa 1943 miaka 26 baadaye na shule na hospitali zilifata misheni.

Kama watu wote waliotawaliwa na wageni na kunyanyaswa, kutawaliwa na wageni wa Kihaya chini ya Wajerumani kuliwaathiri kujiheshimu, nakujitambua kama wanyambo. Kujifunza elimu na dini kwa njia ya kuhemea katika lugha zaidi ya Kinyambo kiliathiri sana Kinyambo,Waumini na wanafunzi walizoea kusikia makatekista na walimu wakifundisha kinyambo kibovu kilichoathiriwa na lafudhi na misemo ya kabila la wahaya.

Bila kutaka wasomi walijikuta wakiathiri matumizi ya lugha yao ya kinyambo kwa jeuri kutokana na wingi wa mashule ya dini, serikali.Jumla ya yote ni kwamba kuanguka umaarufu wa Karagwe ghafla wakati wa kuja kwa ukoloni, kulitekeleza mazingira ya kuathiri kinyambo mpaka wanyambo wenyewe wakawa kama wamemezwa na Wahaya ,kabila ambalo hakukuwepo kabla ya ukoloni.

WANYAMBO KABILA LISILOJULIKANA

Katika miaka ya hivi karibuni kabila la wanyambo limeendelea kuathirika kutokana na taarifa zinajitokeza kila siku kwa wanyambo kubughudhiwa kutika Idara ya Uhamiaji kwa sababu baadhi ya Maofisa wake hawajui kwamba kabila hilo lipo.


Hofu iliyopo ni kwamba hata wanyambo wenyewe hasa waishio nje ya Karagwe hawana ufahamu kama wao ni wanyambo au ni wahaya kwa sababu baadhi yao hujitambulisha kama ni wahaya na wanajaribu hata kuigiza lugha yao. Historia ya Wanyambo haijatafitiwa kwa kina na hivyo hakuna machapisho ya kutosha yanayoelezea historia ya Wanyambo.Yapo machapisho machache sana hasa ya Profesa Katoke na hadithi za wapelelezi kana Hans Mayer ambayo hayako sokoni tena na yaliyopo hayatoshelezi mahitaji.

Mila na desturi za Wanyambo ziko hatarini kutoweka ikiwa ni pamoja na ngoma za asili, nyimbo ,misemo ,majigambo,hadithi na taratibu za maisha nyingi zimetoweka na zilizobaki ziko hatarini kupotea kabisa. Mfano mzuri ni ngoma ya Amakondere ambayo imebaki ikichezwa na kundi moja tu la wazee waishio Rwanyango ambazo hazijarekodiwa ambapo itakuwa vigumu kuruthishwa kizazi kimoja hadi kingine.

Aidha uwepo wa ngoma ile unategemea sana uhai wa wazee hao hata ala za muziki wa ngoma hizo (Amakondere) hazilimwi tena na huenda mmea huu umeshatoweka kabisa.Kwa upande wa lugha ya wanyambo (Orunyambo) imeanza kupoteza uhalisia wake kutokana na mwingiliano na kutozungumzwa mara kwa mara hivyo huenda ikapotea kabisa. Kwa ujumla wanyambwa wanapata usumbufu katika kujitambulisha hasa wanapohitaji baadhi ya huduma katika Wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu hudhaniwa jamii ya wanyambo ni wakimbizi kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda.


HITIMISHO
Kuna haja ya kuweka mikakati ya kufanya utafiti ili kubaini mila, desturi na tamaduni za Wanyambo zilizo njema na kuzihifadhi kwa njia ya maandishi ili ziweze kurithishwa kizazi hadi kizazi na zitumike kwa manufaa ya jamii nzima.Kila la Kheri Wanyambo.

Ni muhimu kuonyesha mila, desturi na mienendo yao mbalimbali ili Wanyambo wenyewe na jamii nyingine ziweze kuelewa ,kuheshimu na kuthamini Utamaduni wa wanyambo hivyo kukuza uelewano wa kitaifa. Wanyambo na jamii nyingine zitaweza kujifunza aina mbalimbali za mila na desturi za Wanyambo zinazofaa kudumishwa, kuboreshwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Kuna umuhimu wa kuwa na siku ya Utamaduni wa Mtanzania na kutoa nafasi kwa jamii moja baada ya nyingine kati ya jamii nyingine tulizonazo kuonyesha mila, desturi na mienendo yao mbalimbali ya jadi ili jamii nyingine ziweze kuelewa na kuthamini utamaduni wa watanzania wenzao. Kujifunza na kufahamu aina mbali mbali za mila na desturi zinazofaa kudumishwa, kuboreshwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kama utamaduni wa Taifa. 


EDITED BY;
Rodrick Wilbroad Mugishagwe

CHANZO
Happiness Katabazi blog


1 comment:

  1. Hi...
    ninawasihi mfanye hima ili muweke habari kuhusu clans za wanyambo na tabiya za kila ukoo!! Pia ninaomba muonyeshe wazi mahali koo za kinyambo zilikotoka...
    Shukran

    ReplyDelete