Tuesday, February 15, 2011

WACHAMBUZI WANAVYOSEMA KUHUSU KUCHAGHULIWA KWA LOWASSA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA.

KUCHAGULIWA kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, kuwa Mwenyekiti wa Kamati nzito ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kumethibitisha nguvu kubwa aliyonayo mwanasiasa huyo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Wachammbuzi mbalimbali katika mtandao maarufu wa JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii kama FaceBook na Twitter, wameelezea uamuzi huo wa wabunge wa kumpa madaraka Lowassa na wabunge wengine ambao ni maswahiba zake, ni hatua muhimu kuelekea 2015.
Mmoja wa wachambuzi hao, ‘Fareed’yeye ameanika wazi kwamba uamuzi huo wa wabunge umetoa nafasi kubwa kwa mafisadi ambao sasa watafanya watakavyo ndani ya Bunge.
Fareed yeye anatoa sababu zifuatazo;
1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.
2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings (taarifa za usalama) na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.
3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye anakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.
4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.
5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.
6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa kina Rostam kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa TLP na UDP ambao ni vibaraka wa CCM kama CUF.
Lowassa, January na Serukamba na wapambe wao wa kamati za upinzani (Zitto, Augustino Mrema, John Cheyo) wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati za Bunge. Watakuwa na majority vote kwenye kamati ya uongozi wa Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana uwezo wa kuamua moja kwa moja shuhuli za Bunge, kanuni, miswada, mwenendo na hoja mbali mbali za Bunge.
Spika Anne Makinda aliyehakikisha kina Lowassa, January, Serukamba na wengine wanapita kuwa kwenye kamati hizi anatajwa kuwa anapokea maelekezo ya Rostam Aziz anayetajwa kuwa ndiye aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.


Mchambuzi mwingine anayejiita ‘Kagemro’ alikua na haya ya kusema:
Kutokana na mambo ambayo leo yametokea mjini Dododma ni dhahiri kuwa kumekuwa na mapinduzi ya wazi ya kuliteka Bunge letu na kuanzia sasa litakuwa halina nguvu tena za kuwawajibisha mafisadi wala hakutakuwa na mtu wa kuzungumza lolote juu ya Mafisadi na ufisadi.
Nayasema haya kutokana na mambo yafuatayo;
1.       Uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge ni kama ifuatavyo;
(i)      Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ni Abdallah Kigoda
(ii)    Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na utawala ni Pindi Chana
(iii)   Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ni Edward Nyoyai Lowassa
(iv)  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ni Magreth Sitta
(v)    Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ni Jenista Mhagama
(vi)  Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ni ………….
(vii) Mwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo na maji ni Prof.David Mwakyusa
(viii) Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu ni Peter Serukamba.
(ix)  Mwenyekiti kamati ya hesabu za za serikali za mitaa ni Augustino Mrema.
(x)  Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma ni Zitto Kabwe
(xi) Mwenyekiti wa kamati ya heswabu za serikali ni John Momose Cheyo.
(xii) Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara ni Mahamoud
(xiii)  Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ni January Makamba.
Baada ya kuwaangalia wenyeviti hao ni kuwa kamati ya uongozi ya Bunge huwa ina wajumbe ambao ni wenyeviti wote kamati za kudumu pamoja na wafuatao;
(i)   Spika –Anne Makinda
(ii)  Naibu Spika- Job Ndugai
(iii)  Kiongozi waUpinzani- Freeman Mbowe.
(iv)  Mwanasheria Mkuu wa Serikali- Fredrick Werema
(v)  Waziri wa Nchi Bunge na uratibu- Willium Lukuvi.
Hivyo basi utaona kuwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo ina wajumbe 18 .
Kazi za kamati ya uongozi ya Bunge ni;
(i)  Kuendesha bunge siku hadi siku
(ii) Kuamua ni hoja gani zipelekwe Bungeni kujadiliwa
(iii) Kuamua nini kifanywe na Bunge na nini kisifanywe na Spika huwa ni msemaji wake wakishaamua.
Hivyo basi kati ya wajumbe 18 wa kamati ya uongozi ambayo kimsingi ndio Bunge lenyewe utaona kuwa Edward Lowassa amejigeuza na kuwa yeye ndiiye atakuwa anafanya maamuzi yote ndani ya Bunge na kuamua lipi lifanyike na lipi lisifanyike kwani wajumbe 13 wanamuunga mkono yeye ama ni watu wake. hao ni pamoja na ;
(i)      Lowassa
(ii)    Cheyo
(iii)   Serukamba
(iv)  January
(v)    Pindi Chana
(vi)  Jenister
(vii) Mrema
(viii) Zitto
(ix)  Makinda
(x)    Ndugai
(xi)  Lukuvi
(xii) Werema
(xiii)  Mahamoud (mbunge wa Kilwa Kasikazini)
Hivyo utaona jinsi Bunge lilivyotekwa.
Lowassa sasa ataweza kufanya yafuatayo;
(i)      Kumuita Membe na kumpa maelekezo ya kibunge
(ii)    Kumuita Sitta na kumpa maelekezo
(iii)   Kuita upya hoja ya Richmond kupitia January
(iv)  Kumuita Magufuli na Mwakyembe kupitia Serukamba
(v)    Kumuita IGP, DG-TIS kumpa briefing kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
Hivyo hii inaonyesha kuwa tutakuwa na Bunge la kumi la aina gani.
Yafaa kila mmoja akatafakari na kuchukua hatua nini kifuate baada ya hapo!

SOURCE: FIKRA PEVU

No comments:

Post a Comment