Friday, October 08, 2010

Karagwe hapatatosha KAHANGWA ndani ya ulingo


Kulingana na taarifa ya TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mwezi uliopita ilieleza kuwa imetupilia mbali pingamizi alilowekewa mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe kupitia Chadema, Deusdedith Kahangwa. Awali Kahangwa aliwekewa pingamizi hilo na CCM na NCCR Mageuzi ambavyo vilidai kuwa mgombea huyo hakudhaminiwa na chama chake na kuwa alijaza majina yake katika sehemu iliyotakiwa kujazwa na Katibu wa chama hicho. Madai mengine katika pingamizi hilo ni kutodhaminiwa na wanachama, ambayo yamepuuzwa na Nec kuwa hayana msingi. “Kama wanachama walirubuniwa kumdhamini, basi walipaswa kupeleka malalamiko yao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya pingamizi kupelekwa kwa msimamizi huyo,” ilieleza barua hiyo ya Nec. Kuhusu madai kwamba mgombea hakudhaminiwa na wapiga kura, Nec imesema kuwa fomu zinaonesha kuwa Kahangwa amedhaminiwa na wapiga kura 31 na msimamizi wa uchaguzi alithibitisha hivyo. Kushinda rufaa kwa Kahangwa jimboni humo, kunatazamiwa kuleta chachu ya ushindani wa kisiasa kwani Chadema inaonekana kuwa na nguvu zaidi ya vyama vingine vya upinzani jimboni humo.

WANA KARAGWE TUUNGANE KWA PAMOJA KUMCHA BWANA DEUSDEDITH KAHANGWA KAMA MBUNGE WETU WA JIMBO LA KARAGWE..

1 comment:

  1. Habari hii ilichapishwa na gazeti la Habari leo la tarehe 07/09/2010 http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=9878&cat=kitaifa

    ReplyDelete